- Home
-
- HAYA NDIYO MAJIBU YA MISS TZ KUHUSU KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ
HAYA NDIYO MAJIBU YA MISS TZ KUHUSU KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo.Madai mazito! Mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss
Tanzania 2011/12 ambaye alianza harakati za kunyakua taji hilo akitokea
Mkoa wa Shinyanga na baadaye kutwaa Taji la Miss Kanda ya Ziwa, Glory
Samwel anadaiwa kumchokonoa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile
kinachodaiwa kuwa ana ukaribu wa ‘kimalovee’ na mpenzi wa Zari, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’.Chanzo cha ‘unyunyuzi’ huo kilitonya
kwamba, mlimbwende huyo amekuwa akionekana mara kwa mara akijivinjari na
Diamond jambo ambalo wadau wamelishtukia na kubaini kuwa ana mpango wa
kuingilia penzi la Zari na kusambaratishia uchumba wa wawili hao.Ijumaa
Wikienda lilinyetishiwa habari hizo hivi karibuni na kuamua kuzifanyia
kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza kujiridhisha kwa baadhi ya matukio
ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa akipiga na Diamond.
Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’.Mbali na picha pia kuna matukio ya sherehe za
‘bethidei’ ambazo Diamond alionekana akiwa karibu na mrembo huyo.Ukiachilia
mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo kwa lengo
la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa na ukaribu
na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo si wa
kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.“Hizo picha za karibu zaidi ni
zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa Diamond aitwaye
Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam) Kijitonyama (Dar)
hivi karibuni.“Ni kweli watu wengi wananituhumu kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana naye kawaida tu,”
alisema Glory.Kwa upande wa Diamond aliliambia Ijumaa Wikienda
kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi wake na anachokijua ni
shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.“Glory
ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu wengine,
suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema
Diamond.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News