HAPATOSHIII!!!! AUNT EZEKIEL NA DADA’KE WEMA PACHIMBIKA

Admin Updates9 years ago5 Views


Dada wa Wema aitwaye Nuru Sepetu.
Hali si shwari! Lile bifu la mastaa wawili wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu ‘Madam,’ limechukua sura mpya baada ya Aunt na dada wa Wema aitwaye Nuru Sepetu kuzua kizaazaa na kuchimbana mikwara.
Kwa kujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati kwenye klabu moja ya usiku jijini Dar ambapo ilisemekana kwamba Nuru aliyefuatana na Wema ndiye aliyeanza kumpasha Aunt baada ya kumuona akiingia na kundi lake.
Ilielezwa kwamba, awali, Aunt alionekana kutomjali Nuru, jambo lililompandisha hasira Nuru na kujikuta akitoa lugha ya matusi.
Baada ya matusi ya Nuru kuwa ‘too much’ (kuzidi), Aunt alivunja ukimya na kumtaka anyamaze lakini dada huyo wa Wema aliendelea kumtusi.

Aunt Ezekiel Grayson.
Ilidaiwa kwamba, kitendo cha Nuru kuendelea kutukana kilimfanya Aunt amrudishie matusi huku wakichimbana mikwara ndipo Wema ambaye naye alikuwa ukumbini humo akawa anamsihi dada yake aache matusi.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na Aunt ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba kama watu wasingewahi kuwatuliza, wangeng’oana meno, kisa kikielezwa kwamba ni kitendo cha yeye (Aunt) kutomsalimia Wema na timu yake.
Kwa muda mrefu sasa, Wema na Aunt ambao walikuwa mashosti wa kufa na kuzikana wamekuwa kwenye bifu lisilojulikana mwisho wake na sasa kinachoonekana ni kwamba limekuwa la kifamilia zaidi.

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.