Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff, akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa RISE kutoka kwa timu inayotekeleza mradi huo mkoani Iringa leo tarehe 13 Machi,2024. Mradi wa RISE unatekelezwa mkoani Iringa katika wilaya ya Iringa na Mufindi, barabara zitakazonufaika na mradi huo ni barabara ya Wenda -Mgama Km 19 na barabara ya Mtili -Ifwagi Km 14 zote zinajengwa kwa kiwango cha lami.