Msanii wa filamu na muziki, Baby Joseph Madaha
Stori: MAYASA MARIWATA
Msanii
wa filamu na muziki, Baby Joseph Madaha amesema ana wasiwasi na afya ya
mwanaume Mkongo anayefahamika kwa jina la Mwani aliyewahi kuwa mpenzi
wa Jacqueline Wolper.
Akizungumza na
Ijumaa hivi karibuni, Baby Madaha alisema, hofu yake hiyo inatokana na
namna mwanaume huyo anavyotapanya pesa huku akitangaza dau kubwa ili
kuwapata mastaa wa kike.
Mkongo anayefahamika kwa jina la Mwani aliyewahi kuwa mpenzi wa Jacqueline Wolper.
“Kimsingi
mimi nina wasiwasi na afya yake, asije akawa anataka kutumaliza. Mimi
simhitaji hata kama ana mamilioni yake. Hofu yangu ni hii tabia yake ya
kutaka kutupitia sisi mastaa, wanaokubali kuwa naye eti kisa ana mkwanja
nawaonea huruma,” alisema Baby Madaha