Pati
hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibwena Bongo ilichukua nafasi kwenye
Ukumbi wa Msasani Beach, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo
shughuli nzima ilikuwa imeandaliwa kama harusi ambapo kwa mujibu wa
waandaaji iliteketeza mamilioni ya shilingi yanayodaiwa kumwagwa na baba
mtoto lakini mwenyewe akaingia mitini.
Kilichoweka rekodi kwenye sherehe
hiyo ni pamoja na vinywaji na misosi ambayo waalikwa walikula na kunywa
hadi wakasaza huku mama mlezi wa wasanii, Mama Loraa akivua saa yake ya
mkononi ya dhahabu na kumpa mtoto huyo ambaye alikuwa akilia.
Baadhi
ya mastaa waliotinga ni pamoja na Kajala Masanja, Halima Yahya
‘Davina’, Salome Urassa ‘Thea’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mama Loraa,
Zubery Mohamed ‘Niva’, Jimmy Mafufu, Herieth Chumila na wengine wengi
ambao walifanya sherehe kufana vilivyo ambapo walikula na kunywa hadi
baadhi yao wakawa ‘bwi’