DKT. ABBAS AITAKA MAKUMBUSHO KUONGEZA UBUNIFU KATIKA ENEO HILI ,SOMA ZAIDI HAPA

Admin Updates2 years ago6 Views

 

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas ameitaka Makumbusho ya Taifa la Tanzania kuimarisha uhifadhi na utangazaji wa makumbusho na malikale ili kuhakikisha zinajulikana kitaifa na kimataifa.

 Dkt. Abbas ameyasema hayo Aprili, 11,2023 Jijini Dar es Salaam, alipokutana na menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja juu ya uhifadhi na utangazaji wa Makumbusho na Malikale nchini.

Amesema kazi ya uhifadhi katika makumbusho na malikale ni kazi ya kiroho inayomkumbusha binadamu alikotoka na anakokwenda kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo, hivyo, suala la uhifadhi endelevu na utangazaji ni muhimu.


“Mwelekeo wa Wizara yetu kwa kipindi hiki na kijacho ni uhifadhi na utangazaji wa makumbusho na malikale ili watu wajue tunachosimamia,” amesema Dkt Abbas.

Aidha, ameitaka Makumbusho ya Taifa nchini pale inapotafuta rasilimali na watalaam mbalimbali katika uendeshaji wa makumbusho na malikale lazima wazingatie masuala muhimu ya uhifadhi na utangazaji.

Licha ya Kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa uhifadhi wa urithi wa Historia, Dkt. Abbas ameitaka Taasisi hiyo Kufanya kazi kwa bidii na kuongeza ubunifu katika utangazaji hasa kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii katika kutangaza fursa za utalii zinazopatikana katika Makumbusho na Malikale.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.