DIAMOND, WEMA , AUNT EZEKIEL NDANI YA MCHEPUKO MKALI: WAZUNGUKANA KIMAPENZI : SOMA ZAIDI

Admin Updates10 years ago4 Views


Ni
tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya
kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye
mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya
kukujuza.

Mastaa
watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.

KILA KUKICHA

Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.

AUNT NA MOZE IYOBO

Duru za kihabari
zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho
huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa
na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze
Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo
akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo
wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.

Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.

AUNT KIOO CHA JAMII?

“Dah! Natambua kuwa
msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo
cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,”
alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za
nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala
jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa
na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni
shosti wa Wema.

Alisema
kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu
waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na
alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.

“Unajua kwa nini nasema
Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale
anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja
kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?”
alihoji Said.

‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.

WEMA NA DIAMOND

Uchunguzi ulionesha
kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’
(Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji
wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.

KAJALA ANAINGIAJE?

Ilibainika pia kwamba
Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke
wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa
hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia
huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema
mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.

‘Petit Man’ akipozi kimahaba na Kajala Masanja, ‘K’.

STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO

Hivi karibuni kwenye
Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo
Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na
kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa
ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika
akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa
kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.

“Unajua
wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti
na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani
wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve
akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.

‘Petit Man’ yule yule akiwa na dada yake ‘Diamond Platinum’, Esma.

NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA

Akiendelea kumpasha Aunt,
jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi
kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema
ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na
Moze na Petit Man amuoe Esma.


“Unajua
hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao  wa
Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama 
unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze
Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man
ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.

Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.

AUNT AWA MBOGO

Baada ya Steve kutoa
dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa
amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi
kumuacha.
“Hata uongee nini Steve,
siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema
kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze
wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.

KUTOKA IJUMAA


Ni kweli wasanii ni kioo
cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale
yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na
kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.