
MSANII wa Bongo Fleva, Nassib Abdul
(Diamond Platnumz), amesema ujauzito aliobeba Zarina Hassan ‘Zari’
anaona kama amewekwa kwenye kiganja cha mchumba wake huyo.
Diamond
alisema licha ya kutokuwa na fikra ya kuwa na maisha ya kujenga familia
na msichana huyo wa Uganda, ila ujauzito alionao unaotarajiwa kumletea
mtoto umekuwa chachu kubwa ya kuongeza mapenzi kwa Zari.
“Sikutegemea
kuwa na Zari, lakini kwa hali aliyonayo sasa ya ujauzito ni kama
ameniweka kiganjani na sasa ninachoomba mtoto azaliwe salama na awe na
akili nyingi,’’ alisema Diamond.
Diamond aliongeza kwamba wasichana wengi aliowahi kuwa na uhusiano nao walikosa vitu vya kufanana naye.
“Niliokuwa
nao nadhani kulikuwa na vitu ambavyo havikukamilika, ndiyo maana
hatukuwa tukiishi kwa muda mrefu na kuanzisha maisha kama haya na
Zari,’’ alisema Diamond.