DIAMOND, NAY ‘WAWAVUA NGUO’ WEMA, SIWEMA HADHARANI!..CHEKI WALIVYOFANYA

Admin Updates10 years ago5 Views

Diamond na Nay wa Mitego wakiimba ngoma yao ya Muziki Gani.
Musa Mateja
DONGO! Wakali wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
wameamua kuwavua nguo waliokuwa wapenzi wao kwa kuandaa wimbo ambao
unazungumzia matendo machafu waliyowahi kutendewa na wapenzi wao hao.
Ngoma
hiyo inayofahamika kama Mapenzi Pesa ambayo inaachiwa leo katika vituo
mbalimbali vya redio, mastaa hao wameimba kwa staili ya kubishana kwa
kuambiana kuwa mapenzi ni pesa mwingine akisema si pesa ila ni
kupetipeti. Mashabiki
wakijiachia. Akizungumza na Risasi Vibes, mmoja wa watu wa karibu na
wasanii hao alisema kwamba, Diamond na Nay wa Mitego, wameamua
kuvunja ukimya kupitia wimbo huo ambapo wamezungumza mambo yote
waliyowahi kutendewa na wapenzi wao ikiwa kama njia ya kutoa kilio chao
kwa jamii ambayo ilikuwa ikiwaona wao kama ndiyo wakosaji baada ya
kutofautiana nao.
“Wameurekodi makusudi kabisa kufikisha ujumbe kwa
mashabiki wao hasa ambao wengi hawakuweza kujua visa vya wasanii hao
kuachana na wapenzi wao na kikubwa zaidi ni kuonesha kuwa mtu hata kama
una pesa kiasi gani au unaonesha upendo wa aina gani lakini kama
mwanamke akiamua kufanya yake, anafanya tu,” alisema mtu huyo wa karibu.

Risasi Vibes baada ya kunasa ishu hiyo, iliwasaka Diamond na Nay ili
waweze kuzungumzia wimbo huo na kueleza ni kipi kilichowafanya hadi
wakaamua kuingia studio na kuimba mambo ambayo kila mmoja yamemtokea
kutoka kwa mpenzi wake. Majibu yao yalikuwa hivi:
“Kiukweli
niliguswa sana baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wangu Siwema hasa
kutokana na namna tulivyoachana, hapo ndiyo nilijua kuna baadhi ya
wanawake hata uishi naye kwa mapenzi yapi na umpatie pesa kiasi gani
bado suala la kutulia linategemeana na yeye tu anavyochukulia,” alisema
Nay.

“Naweza kusema kuwa watu wanatakiwa kuelewa kuwa sisi ni
wasanii hivyo kuna muda inatakiwa kabla hujaimba jambo kuhusu wengine
basi kuna muda mzuri pia ambao tunatakiwa kuimba kuhusiana na mambo
ambayo sisi wenyewe tumefanyiwa ili kuwafahamisha mashabiki wetu, najua
kupitia wimbo huu kuna watakao tuelewa na wengine wataona kama tumeongea
mambo ya chumbani sana lakini ukweli utabaki tu kuwa sanaa ina namna
nyingi ya kufikisha ujumbe kwa mashabiki, hivyo naomba mashabiki wakae
makao wa kula Jumatano (leo) watapata kila jambo ndani ya wimbo wetu
huo,” Diamond.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.