Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya
vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna
aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi
tena!
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara
Diamond amekuwa akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza
kwamba pamoja na kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha
lakini hata kama ‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko
kurudiana na Wema.
“Diamond amekuwa akisema kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na
matatizo aliyokumbana nayo katika uhusiano wake kwa Wema, ni vigumu sana
kurudiana naye wala kuwaza kama ipo siku anaweza kuwa naye, maana
hakuna tena jambo geni asilolijua kwake,” kilisema chanzo hicho na
kufunguka zaidi:
“Kama hiyo haitoshi, Diamond anasema anaposema haoni kitu kipya kwa
Wema anamaanisha ndiyo maana utaona leo hakuna hata siku moja ambayo
amewahi kuwaza kurudiana naye hata kama atatumia ushawishi wa fedha kwa
kumpelekea makontena ya fedha, hawezi kukubali anasema bora afe maskini
kuliko kushea kitanda kimoja na Wema.”
DIAMOND ATHIBITISHA
Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kukutana na
Diamond uso kwa uso ambaye alithibitisha taarifa ambazo zilielezwa na
mtu wake wa karibu:
“Umeambiwa na nani hayo? Sipendi kuongelea sana hivi vitu lakini huo
uliousikia ndiyo ukweli. Kwa sasa nawaza maisha yangu na mpenzi wangu
Zari baada ya kupitia majaribu mengi kimapenzi enzi hizo.
“Huenda wengi wasiamini ninayosema lakini nafsi yangu haijawahi
kuniongoza kukumbuka ya nyuma tena kama ilivyowahi kutokea awali.
“Wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili lakini sikupenda kujibu
kwa kuwa nilihisi litaleta tafrani kwa mashabiki wangu, sioni sababu ya
kuendelea kuulizwa kwenye media hivyo ukweli ni kwamba siwezi kurudi
nyuma tena,” alisema Diamond
ASISITIZA KWA KUREKODI WIMBO
Kuonesha kweli amedhamiria kutogeuka nyuma, Diamond alisema kwa sasa
yuko bize studio kurekodi wimbo na Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki)
ambao utakuwa umesheheni majibu ya maswali yote ya kila kitu ambacho
kilimkera kwenye uhusiano wake na Wema.“Naomba mashabiki wangu wawe na
subira kwa maswali hayo yote, majibu yake yatapatikana katika project
yangu na Nay inayokuja muda si mrefu,” alisema Diamond.
WEMA AJIBU MASHAMBULIZI
Alipotafutwa Wema kuhusiana na kauli hiyo ya Diamond, naye alijibu
mashambulizi kwa kusema kamwe hawezi kurudiana na Diamond, hamfai hata
kidogo na hata akimshawishi na fedha nyingi kiasi gani hawezi kurudi
nyuma.
“Hata aje na Bill Gates (tajiri mkubwa duniani), aje na matajiri wote
anaowajua yeye duniani kamwe siwezi kulamba matapishi, kwanza sitaki
kukumbuka kabisa kuhusu huyo mtu, please naomba nisimuongelee kabisa
huyo mtu,” alibwatuka Wema.
WAMEFIKAJE HAPA?
Wawili hao ambao walidumu kwenye uhusiano na kupamba vyombo mbalimbali
vya habari, kila mmoja amekuwa akimtuhumu mwenzake kuwa msaliti lakini
sababu kubwa ambayo Diamond amekuwa akiisimamia juu ya kummwaga Wema ni
baada ya mrembo huyo kuhongwa gari na mwanaume mwingine.