CELEBRITIES ZONE; TWEET ZA DAVIDO HAZIMLENGI DIAMOND, WAKO POA ASEMA MENEJA
Kwa
mujibu wa mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz, tweet zenye hasira
zilizoandikwa na Davido jana hazimhusu muimbaji huyo wa ‘My Number One.’

Mitandao mikubwa ya Nigeria ikiwemo Pulse na News24
imeandika kuwa tweets hizo ambazo Davido anamzungumzia mtu asiye na
shukrani kwake na kwamba kiama chake kinakuja, zimemlenga Diamond.
Meneja wa Diamond, Salam aka ML Eight ameiambia Bongo5 kuwa hakuna ugomvi wowote uliopo kati ya mastaa hao na kwamba wako poa.
Uhusiano
kati ya mastaa hao wawili uliingia dosari siku ya fainali ya shindano
la Big Brother Africa ambapo baada ya Idris kushinda Davido alitweet
‘And They Cheat Again’ na Diamond ambaye usiku huo alishinda tuzo ya
TFA za Nigeria aliijibu kwa ujumbe wa kuibeza.
Kufuatia tweet hiyo ya Davido, watanzania wengi walimshambulia kwa matusi na kumtaka aombe radhi kitu ambacho aligoma kufanya.
Tangu
hapo, kumekupowepo na speculations kuwa uhusiano kati ya wawili hao
umevunjika na ndio maana imekuwa rahisi kwa wengi kuhusi tweet hizo za
jana zimemlenga Diamond.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News