BUSU LA MWANAUME KWA MWANAUME KWENYE TELEVISION YA TAIFA LAZUA KIZAA ZAA

Admin Updates10 years ago7 Views

Watu wa jinsia moja wakipigana busu

Waandaaji wa kipindi
maarufu cha tamthilia nchini Angola wameomba radhi baada ya sehemu ya
Tamthilia hiyo iliyoonyesha wapenzi wa jinsia moja wakibusu kuamsha
ghadhabu miongoni mwa watazamaji.


Televisheni ya Taifa imesema imesitisha Matangazo ya Tamthilia ya Jikulumessu kwa sababu za kiufundi.


Watazamaji wengi wanaona
kuwa kipindi hicho kilivuka mipaka kwa kuonyesha wanaume wakibusu,
ingawa haijatangazwa kuwa mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja nchini
Angola ni haramu.


Kipindi hicho kilikuwa kinatengenezwa na Kampuni moja inayomilikiwa na Mtoto wa Rais.


Jose Eduardo Paulino dos
Santos,Msanii maarufu nchini humo amekuwa akishutumiwa kunadi vitendo
vya mahusiano ya jinsia moja miongoni mwa Jamii ambayo imekuwa katika
misingi ya kuheshimu maadili na dini.


Kampuni yake,imesema inapitia tena vipindi vyake na imeomba radhi kwa kuwakera Watazamaji.


Kipindi cha Jikulumessu
huangazia maswala yanayogusa jamii kama vile ndoa za mitara, mahusiano
ya jinsia moja, biashara ya ngono kwa ajili ya kuzua mjadala kwenye
jamii.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.