BORA MNIUE ILA UKWEIL NATAKA KUZAA NA DIAMOND PLATNUMZ..AFUNGUKA STAA WA MUVI ZA KIBONGO

Admin Updates10 years ago5 Views



 Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ akipozi.

BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza
na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini
Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka
kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote
kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.

MAKUBWA!
Alidai
aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo
anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).

“Ndugu
wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote
kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa
bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni
kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa
kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke
inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti
Lulu.

Pamoja
na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti
ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.

Mkali wa Bongo Fleva ‘Diamond Platinum’ akiwa na mpenzi wake wema Sepetu.

IMANI
Anti
Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali japokuwa hawajawahi
kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba walishakutana na
kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii…
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?

MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond
hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni
halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku
hiyo alinisifia.

“Niliambiwa
alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni zuri hivyo
naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye aliwahi
kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.

BIFU?
Anti
Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba Wema atakasirika,
hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha naye bifu zito.

 
‘Diamond Platinum’ wakati akiwa na Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Alisema
kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba kikubwa anataka
kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja aendelee na maisha
yake.

NENO!
“Najua
Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa sababu nimeamua na yeye
ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.

DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond
aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito aliyekuwa mpenzi wake, Penniel
Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda mfupi ilidaiwa kuchoropoka.Pia
aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema ambaye naye ilidaiwa
ilichoropoka.

Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
SWALI LENYE HOJA!
Baadhi
ya watu waliomsikia Anti Lulu akitangaza ishu hiyo walijiuliza swali
moja tu: ‘Hivi kweli Anti Lulu huyuhuyu anaweza kuwa mama bora?’Diamond
hakupatikana ili kufikishiwa ujumbe huo na kujua namna alivyopokea
taarifa hiyo ya Anti Lulu. 

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.