1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo
mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI
TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa
hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea
kupotea nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana
na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na
kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume
kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi
kazi kabisa!”
2 :
UJUZI
Wanawake wengi hasa
waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi
kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya
mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo
anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano
toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo
wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume
ajione kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda
sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza
uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo
kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya
mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali
amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa
vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi
huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
3:USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume
matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa
mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa
mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu
wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
4:GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa
nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala
miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni
mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza
kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha
kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko
wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
5:USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha
mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi
au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye
humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
Chanzo:Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha
California
weka maoni yako hapo ktk comment chini