ANGALIA HAWA MASTAA WAKIMPIGIA SALUTI DIAMOND PLATNUMZ

Admin Updates10 years ago5 Views

Na Gladness Mallya BAADA
ya Jumamosi iliyopita msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O zijulikanazo kama
Channel O Africa Music Video Awards 2014 (CHOAMVA), zilizofanyika Afrika
Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa mbalimbali nje na ndani ya
nchi wamempigia saluti.

 
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi .

Diamond ambaye ameweka rekodi nchini kwa
kuwa msanii pekee kuchukua tuzo tatu kwa mpigo huku tuzo hizo zikiwa ni
pamoja na ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Video Bora ya
Muziki wa Afro Pop, Mwanamuziki Bora Anayechipukia hivyo alikosa tuzo
moja tu ya Video Bora kwa mwaka.

Msanii mkali kutoka Nigeria Davido aliyetoa pongezi kwa ‘Diamond Platnumz’.

Katika makala haya tunakuletea baadhi ya mastaa waliompigia saluti
Diamond na kumpongeza kwa hatua aliyofikia.SUNDAY MANGU ‘LINEX’“Ukweli
nampongeza sana Diamond na kikubwa nasema ametisha sana na ametutoa
kimasomaso.”

DAVIDO
“Tanzania
imesimama! Diamond Platnumz ameweza tena!” aliandika mwanamuziki huyu wa
Nigeria kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Msanii wa Hip hop Bongo, Madee akipozi.

EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
 “Diamond anatakiwa kuwa muwazi kwa sisi wenzake ili tuweze kuleta tuzo
nyingi Bongo. Atoe mianya kwa wasanii wenzake kwa kuwaonesha njia kwani
Nigeria wasanii wake walifanikiwa kutokana na mmoja wao alipofanikiwa
aliwaonesha njia ya kujipenyeza kimataifa zaidi.”

 
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
“Kweli Diamond
anastahili kwa sababu anajituma na anafanya vizuri, nampa hongera sana,
aongeze bidii zaidi asibweteke kwa tuzo alizopata.”

WAJE
“Waooh! Hongera mkaka kwa tuzo tatu.” Aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Msanii wa muziki kutoka Nigeria , Waje.

MADEE ALI
“Diamond anastahili kwa kweli, wewe ni
zawadi yetu, sasa hivi neno Bongo Fleva linatajwa Afrika nzima
hakutakuwa tena na maswali mengi ukisema unatoka Tanzania, hongera
sana.”

Katika kuwapa shukrani mashabiki wake kwa kumfanikisha kushinda tuzo
hizo, Diamond atatinga nazo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar
Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar  ambapo pia usiku huo atapiga
shoo ya nguvu.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.