Afungwa Miaka 20 Jela Kisa Vipande 14 vya Nyama ya Pofu

Admin Updates1 year ago5 Views

Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Kijana Mussa Ally Makandaje (32), Mkazi na Kijiji cha Msinjili Wilaya ya Tunduru baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kukutwa na vipande 14 vya nyama ya mnyama aina ya pofu
Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya jinai Na.18 ya mwaka 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Lilian Haule amenukuliwa akisema “Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote”.
Imeelezwa kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo August 10 2023 na kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 25 2023.
Pofu ni Mnyama Jamii ya swala anayepatikana katika mbuga mbalimbali za Tanzania na anatajwa kuwa na mwili mkubwa kuliko wote katika Jamii hiyo ya swala, sifa nyingine ni sura nzuri pamoja na utamu wa nyama yake uliyoifanya kuwa moja ya nyama zinazopendwa sana katika uwindaji

 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.