Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.
Waziri Kairuki amewataka Wakandarasi hao kuzingatia masharti ya mikataba yao na kuhakikisha kuwa hawatakuwa kikwazo kwenye utekelezaji wa mradi huo. Amesisitiza kuwa ofisi yake itahakikisha utekelezaji wa mradi huo unakuwa na mafanikio makubwa na kuepuka dosari zilizojitokeza katika awamu iliyopita.
“Mradi huu unakwenda kutatua kero mbalimbali ikiwamo ujenzi holela wa makazi, miundombinu duni ya usafiri, mabadiliko ya tabia nchi kwa jiji la Dar es Salaam zinazosababisha mafuriko na utupaji taka ngumu ovyo,”amesema Kairuki
Mratibu wa Mradi wa Miradi ya Benki ya Dunia ikiwepo uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP), Mhandisi Humphrey Kanyenye akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo Mei 30,2023 ukumbi wa Mkapa jijini Dodoma.
Picha ikiwaonyesha wabunge mbalimbali wakiwemo Jerry Sillaa wa Jimbo la Ukonga na Saaashisha Mafuwe ni baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taznania walioshuhudia utiaji saini wa mkataba huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni utakaotekelezwa na wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)