Taifa Stars njia nyeupe kufuzu AFCON, Yalamaba Milioni 10 za Rais Samia…Algeria waichapa Uganda bila huruma

Admin Updates1 year ago5 Views

Tmu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepata Milioni 10 kutoka kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama pongezi ya bao 1-0 waliloshinda hii leo kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Niger .

Algeria imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Uganda usiku huu Uwanja wa Omnisport Jijini Douala nchini Cameroon katika mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.

Mabao ya Algeria yote yamefungwa na mshambuliaji wa Lugano ya Uswisi, Mohamed El Amine Amoura dakika ya 42 na 66, wakati bao pekee la Uganda limefungwa na mshambuliaji wa Vyškov ya Jamhuri ya Czech, Fahad Aziz Bayo dakika ya 88.

Kwa ushindi huo, Algeria inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Kundi F kwa pointi nane zaidi ya Tanzania inayofuatia ikiwa na alama 7, wakati Uganda inabaki na pointi zake nne mbele ya Níger yenye pointi mbili baada ya wote kucheza mechi tano.

Mechi za mwisho Septemba 4, 2023, Taifa Stars watakuwa wageni wa Algeria Jijini Algiers na Uganda watakuwa wageni wa Niger Uwanja wa Jénérali Seyni Kountché Jijini Niamey.

 Algeria waichapa Uganda, Stars njia nyeupe kufuzu AFCON

Stars inahitaji walau alama moja tu kukata Tiketi ya kucheza Michuano ya AFCON mwakani.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.