
Hatimaye Kichwa cha James Temba Chapatikana Kitunda
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefanikiwa kupata kichwa cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), James Temba, ambaye mwili wake ulipatikana katika Mto Msimbazi mnamo Aprili 30, 2026.
Akizungumza na Vyombo vya Habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema kichwa kilikutwa kikiwa kimefukiwa katika eneo la Kibeberu, Kitunda Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam
Kamanda Muliro amesema kuwa hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia watu watano kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mganga wa kienyeji, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo halisi cha mauaji hayo ambapo ameongeza kuwa tukio hilo linaweza kuhusishwa na mambo mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina pamoja na masuala ya kimapenz






