Waziri Katambi akutana na Balozi wa China Nchini

Masama BlogMATUKIOSIASAKITAIFA2 weeks ago57 Views

Waziri Katambi akutana na Balozi wa China

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, na kufanya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ikiwemo mbinu za kudhibiti uhalifu, matumizi ya teknolojia katika kuimarisha usalama, pamoja na kupambana na uhalifu unaovuka mipaka.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Mkuu wa Huduma za Urekebu kutoka Jeshi la Magereza, Kamishna Amina Kavirondo, pamoja na Afisa Kiungo wa China katika Kitengo cha Polisi Kimataifa, Makao Makuu ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi (SP) Damas Nyungula.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri, jijini Dar es Salaam.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.