Dkt.Hassan Abbas ahudhuria Mkutano wa 45 wa Kamati ya UNESCO ya Urithi wa Dunia

2 years ago104 Views

Katibu Mkuu, Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi

Katibu Mkuu, Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wataalamu wengine wa Serikali,  leo wamehudhuria Mkutano Unaoendelea wa 45 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO jijini Riyadhi, Saudi Arabia, ambapo pamoja na mambo mengine Tanzania itasisitiza juu kuendelea kuenziwa kwa vivutio vyetu mbalimbali vilivyomo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia ili kuendelea kuvuta watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali kuja nchini. Vivutio saba vya kiutamaduni (cultural) na asili (natural) vya Tanzania ambavyo vipo kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia na mwaka wa kuingizwa orodhani ukiwa kwenye mabano ni:

1. Hifadhi ya Serengeti (1981); 

2. Jiopaki ya Ngorongoro (1979); 

3. Pori la Akiba la Selous (1982); 

4. Mji Mkongwe wa Zanzibar (2000) 

5. Michoro ya Mapangoni Kondoa (2006);

6. Magofu ya Kilwa Kisiwani na Kisiwa cha Songo Mnara (1981); na

7. Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (1987).

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.