
ya leo March 4, inahusu mvutano wa mtoto anaegombaniwa na wanaume
wawili huku kila mmoja akidai ni mtoto wake baada ya mama yake kufariki.
Mama wa hiari wa familia ya mwanaume mzungu amesema kuwa aliwahi
kupata malalamiko kutoka kwa mke wa mzungu kuwa mume wake ana mwanamke
wa kiswahili na amezaa nae mtoto ambae alikuwa akija nyumbani kwake mara
kwa mara akiwa na mama yake hadi walipohama na kurudi Togo, baada ya
mwanaume huyo kusikia mama wa mtoto huyo amefariki akarudi Tanzania kuja
kumchukua walimkatalia na kumwambia sio mtoto wake.
Mama wa kijana wa kiarabu anaedai kuwa baba halali wa mtoto huyo
amesema, kijana wake alikuwa na mahusiano na huyo binti lakini
alipogundua anamahusiano na huyo mzungu aliamua kuachana nae, wakati huo
tayari alikuwa na ujauzito wake baade aliambiwa mtoto huyo sio wakwake
lakini hakukubali wakamtaka wapime DNA jambo ambalo alikataa na kupeleka
swala hilo Polisi.