Mrembo na staa wa bongo movies, Jackline Massawe Wolper ameonyesha
kuchukulia ni kama changamoto kitendo cha msanii wa muziki kutoka kundi
la makomando Fredy Felix ambae ni bwa’mdogo “Serengeti Boy” kujinadi
hadharani kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wolper huku
akielezea njinsi alivyompata na kumsifu kuwa alimpata penzi ambalo
hatoweza kulisahau.
Felix aliyasema hayo hivi juzi kati alipokuwa akifanya mahojiano na
Global Tv online nakusababisha stori hii kuenea kwa kasi sana kwenye
magazeti na blogs za udaku.
Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliandika ujumbe
unaoonyesha kwa namna moja au nyingine kitendo hicho amekichukulia kama
ni changamoto tu za maisha ya zamani.
Wolper aliandika maneno haya kwa lugha ya kimombo
“The past can hurt but the way I see it, you can either run from it or learn from it”.
Kwa tafsiri isiyo rasmi anaamanisha kuwa mambo yaliyopita yanaweka
kuumiza lakini kwa jinsi anavyo yatazama yeye , unaeza kuyakimbia au
kujifunza kutokana yaliyopita.
Mara baada ya ujumbe huu, mashabiki wake wengi walimpa moyo huku
wakimponda kijana Felix kwa kufanya kitendo ambacho wengi walisema cha
kipumbavu.