ILIKUWA KAMA UTANI HIVI,D’BANJ AKABURUZWA MAHAKAMANI

Admin Updates10 years ago6 Views

Dbanj60

Hii ishu ilikuwa kama utani hivi, zikaanza stori kwamba D’Banj
anadaiwa na jamaa mmoja Nigeria.. baadae tukasikia kwamba jamaa
anayemdai ametishia kumshtaki.. leo hii story ina mwendelezo wake.


Henry Ojogho ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Broron Group and MindHub Technologies amesema anaidai Kampuni ya DKM Media ambayo inamilikiwa na D’Banj
kiasi cha kama Naira Mil.60 ambazo ukiziweka kwenye hela yetu ni kama
Tshs. Mil. 600 hivi.. kesi ilifika Mahakamani na kuanza kusikilizwa
Lagos Nigeria, March 30 2015.

Siku hiyo ya kwanza kesi kusikilizwa Mahakamani wote wawili, yani D’Banj mwenyewe pamoja na Henry hawakuwepo Mahakamani.

Kesi ilisogezwa mbele na itasikilizwa tena Mahakamani siku mbili zijazo, yani May 7 2015.. D’Banj ni moja ya mastaa makubwa wenye mafanikio Africa ambaye anafanya kazi za kimuziki Marekani chini ya lebo ya G.O.O.D Music ambayo inamilikiwa na rapper Kanye West.

Kwenye list ya mastaa wa muziki wenye utajiri mkubwa zaidi Africa D’Banj yuko #3.. Hili deni ni kweli kashindwa kulipa au ni nini kinaendelea hapo??

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.