Staa wa Bongo Movie ambaye kwa sasa anaishi ughaibuni, Lucy komba
ameamua kuelezea tuhuma zinazomkabili za kua na uhusiano wa kimapenzi na
Hamad Ndikumana, aliekua mme wa msanii mwenzake Irene Uwoya.Akizungumza
na gazeti la sani Lucy ameelezea kwamba hakuna jambo lolote
linalowakutanisha na Hamad zaidi ya filamu iitwayo “Kwanini nisimuoe”
inayohusisha watu wawili tu.
Lucy alisema walipokua wanarekodi filamu hiyo ndio uvumi mwingi
ulianzishwa. Ingawa mashabiki wengi walipinga kuwa haiwezekani filamu
nzima ikahusisha watu wawili tu na kwamba hao wawili wanauhusiano lakini
Lucy amesema kwamba filamu hiyo ikitoka itatoa majibu yote na
amewasisitiza mashabiki wainunue filamu hiyo ya “kwanini nisimuowe”.