KALI YA MWAKA:ONA JINSI NG’OMBE WALIVYOANDAMANA HADI KWENYE MADUKA MJINI KISA MAZIWA!!

Admin Updates9 years ago6 Views

Ushawahi kukutana na ngo’mbe katika maduka ya jumla?Na ushawahi kusikia maandamano yanayojumuisha ng’ombe ?

Amini usiamini wanunuzi katika maduka ya kifahari katika mji ya Asda Queensway, Stafford Uingereza walipigwa na butwaa ng’ombe walipoingia dukani humo !Yamkini mifugo hao waliletwa humo na wakulima waliokuwa wakiandamana kupinga bei duni ya maziwa wanayolipwa na uongozi wa maduka hayo ya jumla.

Wakulima 70 wakiandamana na ng’ombe wawili walishiriki katika maandamano hayo ya kipekee.
Mnunuzi mmoja Adam Williams aliiambia BBC kuwa hata wahudumu wa duka hilo hawakuficha mshangao uliowakumba.
Walipigwa na butwaa wote ng’ombe walipoingia dukani!”
Walisababisha hali ya mshikemshike kwani walifululiza hadi upande wa ndani kabisa ya duka hilo!”
Wakulima hao wanataka maduka hay ya jumla yawaongezee bei ya maziwa ili na wao waweze kujikimu kimaisha.
Hata hivyo wasimamizi wa maduka hayo ya jumla wanasema kuwa hilo halitafanyika.
Wanadai kuwa hakuna uhusiano wowote wa bei ya juu ya maziwa katika maduka yao na bei duni wanayolipwa wakulima shambani.
Mkulima mmoja kutoka Stafford Matthew Weaver, amenukuliwa akisema
“Tulijua kuwa iwapo tunataka kupata ufanisi katika maandamano yetu ilikuwa lazima tufanye kitu cha kipekee ambacho pia kitawavutia watu na kuwapa sababu ya kuwachekesha.”
Weaver alisema wafugaji hao walitokea Derbyshire, Shropshire na Warwickshire .
Alisema kuwa bado wanapanga maandamano mengine katika maduka zaidi.
Kampuni ya maziwa ya Muller ilitangaza kuwa itapunguza bei ya maziwa kwa sababu soko lake limeporomoka
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.