
Kama wengi mnavyokumbuka siku ya Kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka Mbunge wa Ukonga ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa alikuwa mmoja wa waalikwa waliosali kanisani kwa mtume na nabii Suguye lililopo Kitundu Ukonga Jijini Dar es Salaam.Moja ya mambo yaliyozua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii ni aina ya Simu anayotumia waziri silaa tofauti na wengi walivyotarajia huku waki sema mengi juu ya simu hiyo iliyoonekana pia kuwa tofauti na simu za viongozi na watu wenye majina makubwa kama ilivyozoeleka na wengi.
Katika ibada hiyo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Samia Suluhu Hassan alimpigia simu Nabii Suguye kupitia simu ya Waziri Jerry Silaa na kumpongeza Nabii Suguye kwa Kazi ya Mungu anayoifanya,Pia waziri Silaa alitumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania wamuombee Rais Samia kwa Kazi Kubwa anayoifanya kwa Taifa na watanzania kwa ujumla.






