Kipekee sana nachukua nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kunipa nafasi nyingine ya kutumika chini ya Serikali ya awamu ya sita katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Mwenyezi Mungu akubariki sana mama.
Nakushukuru sana ndugu yangu Mheshimiwa Abdallah Mtinika, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke kwa muda wote tuliofanya kazi kwa pamoja tukisogeza mbele gurudumu la maendeleo la Temeke yetu.
Pia natumia nafasi hii kuwashukuru Baraza la Madiwani, Watumishi na Wakazi wote wa Manispaa ya Temeke kwa ushirikiano kiano wenu kipindi tunafanya kazi kwa pamoja, takribani muda wa miaka mitatu na siku 14. Mungu awabariki sana na tuendelee kufanya kazi kwa bidii sana.