Waziri wa kilimo Mhe, Japhet Hasunga amezitaka bodi zote zilizopo chini ya Wizara yake kuanza kujitathimini kama zimeshindwa kuwaondolea kero ya Rushwa kwa Wakulima zijiondoe kabla ya mwezi wa saba mwaka huu
Kauli hiyo ameitoa akiwa Wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa soko la zao Tumbaku kitaifa huku akisema Wizara hiyo ina mpango wa Kusafisha watu wote ambao Wanaojihusisha na Rushwa na kukwamisha kilimo cha zao hilo
“Mwaka huu tunaanza mabadiliko makubwa ndani ya wizara ya kilimo ili Kusafisha watu waliozoea Rushwa wakafanye kazi sehemu nyingine siyo kilimo na niwaase bodi msiegemee upande wowote ule hakikisheni mnasimamia sheria”Amesema Hasunga
Mwenyekiti wa bodi ya Tumbaku nchini (TTB) Hassan Mwakasavi ameiomba Serikali kuhakikisha inawatafutia masoko ya zao hilo ili Wakulima walime kilimo cha zao hilo wakiwa na uhakika wa masoko yasiyo na Madeni na Usumbufu
“Ombi langu kwa viongozi itendeeni haki zao la Tumbaku ili Wananchi wanufaike na zao hili kwani ni zao zuri linalo stahimili ukame “Amesema Mwakasuvi
Aidha pamoja na kukabiliwa na Changamoto mbalimbali Katika uzalilishaji wa zao la Tumbaku bado linachangia pato la Taifa kwa kuingiza Fedha za kigeni zaidi ya dola za kimarekani Milioni 195.8 Katika msimu wa kilimo cha Mwaka jana.
Waziri wa kilimo Japhet Hasunga akisititiza jambo kwenye Ufunguzi wa Zao La Tumbaku Mkoani Tabora
Pichani ni Shehena ya zao la Tumbaku likiwa kwenye ghala
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/30cmZfw
via
