Taarifa kwamba “WhatsApp inaweza kudukuliwa” sio jambo ambalo mtumiaji yoyote wa mtandao huo wa kijamii anataka kusikia wala kuona katika kichwa cha habari.
Alafu kuongezea kwamba “Wadukuzi walifanikiwa kuweka mfumo wa uangalizi” na kitengo cha habari cha kampuni hiyo wana kibarua kikubwa mikononi mwao.
WhatsApp linasema akaunti kadhaa zililengwa na ” mdukuzi mkuu wa mitandao”.
Lakini iwapo kauli hii imekutia wasiwasi, haya ni baadhi ya mambo unayostahili kufanya kuhakikisha mawasiliano yako yapo salama.
Udukuzi huo uligunduliwa kwanza mapema mwezi huu.
Wakati huo Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatsApp, iliwaambia maafisa wa usalama kwamba lilikuwa : “pengo katika mawasiliano ya sauti ya WhatsApp VOIP [voice over internet protocol] iliyoruhusu udukuzi kupitia vifurushi vya mfumo wa SRTCP [secure real-time transport protocol] vilivyotumwa kwa nambari ya simu ya mlengwa.”
Sawa.
Hebu tulifasiri hilo – ina maana wadukuzi walitumia simu ya WhatsApp kupiga kwa nambari ya mlengwa.
Hata kama simu haikushikwa, mfumo huo wa udukuzi uliidhinishwa kutokana na pengo hilo katika mawasiliano ya sauti ambao hauna usalama wa kutosha.
Simu pengine ilikatika na haionekani kwenye orodha ya waliopiga simu katika simu yenyewe, kwasababu wadukuzi walikuwa tayari wameidhibiti.
KUSOMA ZAIDI BOFYA BBCswahili.com
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HtFGTx
via

