MASTAA wawili waliokuwa mashosti siku za nyuma, Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wameingia kwenye msuguano tena hivi karibuni huku hali ikionesha kuwa mastaa hao kwa sasa ndiyo basi tena.Hali hiyo imetokea juzi baada ya Aunty kuweka picha ya kumtakia siku njema ya kuzaliwa rafiki na msanii mwenzake, Maimartha Jesse kwa kuandika, “Happy bday Kipenzi cha Roho yangu …..Unajua kama Nakupenda cha zaidi Naomba Yesu Akutunze milele.”
Katika post hiyo, followers kadhaa wa Aunty walikomenti akiwemo staa mwenzake kwenye tasnia hiyo, Wema Sepetu aliyekomenti “Yesu atamtunza…” Baada ya hapo, Aunty akaibuka na kumtolea povu Wema akimchana “Achana na mm ww @wemasepetu“ hali iliyoibua maswali na mijadala mingi mitandaoni, huku watu wakitaka kujua kwa nini Aunty amemshushua hivyo Wema.

Inasemekana kwamba, chanzo ni Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Wema kumsema vibaya Aunty kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Kwa hali ilivyofikia mpaka sasa inaonesha sio rahisi tena kwa waigizaji hao kuelewana.
Tangu siku za hivi karibuni, Wema alipokosana na rafiki yake Muna Love na kumsema vibaya kwa kutumia video aliyojirekodi na kuisambaza mitandaoni, Wema kwa sasa amekuwa akijitahidi kuwa karibu na Aunty ili warudishe urafiki wao wa zamani japokuwa jitihada zake zinaonesha kugonga mwamba baada kuambulia maneno mazito kutoka kwa Mama Cookie.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






