Hayo amesema jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya unywaji maziwa shuleni Duniani itakayoadhimishwa Septemba 25 mwaka huu mkoani Iringa.
Mpina amesema kuwa ni mikakati ya serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji wa maziwa unaongezeka kutoka lita bilioni 2.7 hadi kufika lita bilioni 7 kwa mwaka ifikapo 2020.
Amesema kuwa malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025 kila shule ya msingi iwe na programu za kunywa maziwa shuleni na kila mtanzania awe anakunywa angalau lita 100 kwa mwaka.
Kwa sasa kuna shule 25 tu ambazo zinatekeleza Programu ya unywaji maziwa shuleni na kunufaisha jumla ya wanafunzi16.849 kwenye wilaya za Njombe, Mbeya na Wangingo’mbe.
Programu hizi zinaendeshwa kwa ushirikiano na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Viwanda vya kusindika maziwa, wazazi na wafadhili mbalimbali.
Waziri Mpina ametoa pia rai kwa wananchi kunywa maziwa na bidhaa za maziwa ili kuchochea maendeleo ya Tasnia ya Maziwa.
Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa shuleni yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa uwanja wa Samora. Kauli Mbiu ya Maadhimisho haya ni Glasi moja ya maziwa kila siku kwa afya na Elimu bora.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2IaAxkr
via

