Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan imetenga fedha katika bajeti ya mwaka 2023/24 kwa ajili ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya umwagiliaji katika bonde la Mto Ruvuma,Ruhuhu na Litumbandyosi yaliyopo mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Philip Isdor Mpango katika Wilaya za Nyasa na Mbinga,Mkoani Ruvuma.
Akizungumza na wananchi wa wilaya za Mbinga na Nyasa,Makamu wa Rais Dkt. Mpango aliwapongeza wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa mchango wao mkubwa kwenye usalama wa chakula hapa nchini kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka hasa mahindi na kutumia fursa hiyo kuitaka Wizara ya Kilimo ieleze jinsi ilivyojipanga katika utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.
Akitoa maelezo ya Wizara ya Kilimo Naibu Waziri Mavunde alieleza yafuatayo;
-Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya umwagiliaji mkoani Ruvuma ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
-Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali itafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ujenzi wa miumbombinu ya Umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruvuma lenye jumla ya hekta 26,066,Mto Ruhuhu lenye hekta 3,700 na Litumbandyosi hekta 900 pamoja na uchimbaji wa mabwawa makubwa matano(5) na ukarabati wa skimu za umwagiliaji katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma.
-Mkoa wa Ruvuma wamezalisha zaidi ya tani milioni 1 ya mahindi,ni mkoa ambao serikali itawekeza kiasi kikubwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
-Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa soko la uhakika la mazao ya wakulima,na kwasasa Wakala wa Hifadhi ya Chakula(NFRA) wamefungua vituo 17 vya ununuzi wa Mahindi katika wilaya za Mkoa wa Ruvuma.
-Mbolea za Ruzuku zitaendelea kutolewa kama msimu uliopita,na kwasasa tumesajili vituo vingi zaidi vya mauzo ya mbolea ili wakulima wasiifute mbolea umbali mrefu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









