Waziri wa ujenzi ,uchukuzi na Mawasiliano Muhandisi Isack Kamwelwe akimuelekeza mkandarasi eneo LA uwanja lililopo jiji Arusha kwa ajili ya ujenzi Wa jengo LA makao makuu ya mashirika ya posta Kwa nchi za Afrika ,litakalo gharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 33 (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Msimamizi na mshauri wa ujenzi wa jengo hilo Nathanael Alute kutoka kampuni ya B.J. Amuli Architects akitoa maelezo mbele ya Waziri Kamwelwe.
WAZIRI wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano
Akizungumza wakati wa kukabidhi eneo hilom Mhandisi Kamwelwe amesema ujenzi huo umekuja muda muafaka kwa kipindi cha Rais wa Awamu ya Tano Dk.John Magufuli ambaye anafata nyayo za Baba Wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na anaamini kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati
“Kuna nchi 45 wanachama wa mashirika ya Posta katika nchi za Afrika 1980 walikaa na kukubaliana makao makuu ya mashirika ya posta yawe hapa nchini Tanzania na Baba wa Taifa akakubaliana nao na wakapanga yajengwe Arusha na ndio maana katika kuathimisha miaka 40 ya mashirika haya tumeamua tuanze kujenga jengo la makao makuu ya mashirika haya ya posta Afrika” amesema Waziri Kamwele
Amesema jengo hilo litakuwa na gorofa 16 na hadi kumalizika litagharimu kwanba linatakiwa kujengwa na kumalizika kwa kipindi cha miezi 30 huku akimtaka Mkandarasi wa jengo hilo kujenga katika ubora unaotakiwa na viwango vya Serikali .
Amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wafanyakazi wao ambao wanatoka nje ya nchi kuja na nyaraka zote za uhamiaji pamoja na vibali vya kufanyia kazi hapa nchini.
“Jengo hilo ni makao makuu ya mashirika ya posta Afrika, hivyo hairuhusiwi mtu yeyote asiehusika kuingia katika eneo hili bila kibali kutoka kwa wahusika ,eneo hili ni la kimataifa halitakiwi kuingia bila kibali iwapo mtu atakutwa hatua kali za kisheria,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk Jones Kilembe ameishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoonyesha usimamizi na ufuatiliaji hadi kufikia hapa tulipofika katika ujenzi wa jengo hilo la makao makuu ya mashirika ya posta Tanzania.
Amewataka wananchi wa Arusha kutoa ushirikiano katika masuala ya ulinzi hata ikitokea katika eneo la uchangiaji huku akiongeza kuwa watamsimamia vyema mkandarasi huyo na kuhakikisha anamaliza kazi kwa muda uliopagwa na ikiwezekana hata kabla ya muda uliopangwa kufika
Wakati huo huo Mkuu Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameishukuru Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kujenga makao makuu ya mashirika ya posta nchi za Afrika jijini hapa.
Msimamizi na Mshauri Wa jengo hilo Nathanael Alute kutoka kampuni ya B.J. Amuli Architects amesema kuwa atasimamia vyema ujenzi huo uwe wa viwango vinavyotakiwa na serikali ,na kumalizika kwa muda uliopangwa huku akijitaidi gharama za ujenzi zisiwe kubwa zaidi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/303kCME
via






