Waziri Jenista Mhagama afunguka mazito kuhusu DAS Mwampamba,Ampongeza

Admin Updates10 months ago6 Views

 

Na Juma Nyumayo, Songea

Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba  amehimiza kutembelea vivutio vya utalii na kuwekeza wilayani Songea.

DAS Mwampamba Ametoa wito huo akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile kwenye Bonanza la Bank ya CRDB lililofanyika Shule ya Sekondari ya De Paul, Songea.

Bonanza lenye kuhamasisha Watumishi wa CRDB utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo ikiwemo utaratibu wa kupima afya zao kila wakati na kuzingatia lishe Bora.

Mwampamba  ametumia Bonanza hilo kuwahimiza na kuwakaribisha Watumishi hao na wengine wanaotoka  maeneo mbalimbali nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Wilaya ya Songea ikiwemo Bustani ya wanyama pori, Ruhila Zoo, Makumbusho ya Taifa ya vita vya Majimaji  na ya Dkt.Rashid Mfaume Kawawa na alikumbushia kuwa Songea ni Mji wa Kihistoria.

Amewaomba watumishi  wa CRDB na wengine kuwekeza Wilayani Songea kwenye Sekta ya  Kilimo kabla ya kusubiri kiinua mgongo baada ya Kustaafu.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.