Na Mwandishi Wetu. Blog ya Jamii
WATANZANIA wameshauliwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuchochea wazawa kufanya vizuri zaidi kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kampuni ya wa asili asilia Limited ambayo inatengeneza bidhaa za ngozi asilia ya Tanzania Dedan Munis katika viwanja vya maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa.
Amesema kuwa pamekuwepo nakasumba mbaya kwa watanzania kupenda bidhaa za kigeni badala ya kupenda zinazozalishwa na watanzania wezao ambao pia wanatengeneza ajira kwa vijana wa kitanzania.
Alisema iko shida kubwa kwa watanzania kwani wanapenda sana bidhaa za nje kuliko za ndani jambo ambalo linazolotesha bidhaa za ndani ukizingatia kuwa bidhaa hizi zinatengenezwa katika kiwango cha juu na cha ubora tena kwa Mali ghafi za ndani.
“Ndugu waandishi kimsingi nawakaribisha wananchi watanzania wezangu hapa sabasaba katika majengo haya ya Jakaya Kikwete Banda na 31,32waje wapate bidhaa bora zaidi zinazotengezwa na watanzania wenyewe kupitia Kampuni ya waasili asilia limited.” Alisema Munisi.
Nakuongeza kuwa hapo kuna changamoto ya uwepo wa bidhaa Kutoka nje ambazo pia ni za plastiki na Mara zote watanzania ndio wanakimbilia,lakini nivema wananchi wakafika katika Banda hilo la Jakaya kikwete ili kujionea vitu vizuri vinavyozalishwa na wazawa katika kiwango cha ubora.
Amesema mwaka huu wamejipanga zaidi kushinda mwakajana kwani wanabidhaa bora zaidi kama vile viatu vya ngozi aina zote,sandles kwa akina mama na akina Baba na hata watoto mabegi kwa (handbegi) na vitu vingine vingi na tena vinapatikana kwa gharama nafuu.
Amesema katika kumuunga mkono mh.Rais katika azima yake ya viwanda basi wao wamefanya kwa vitendo na ameweza kuajiri watanzania wakutosha tu japo bado changamoto mbalimbali zipo ila wanapambana nazo.
“kama watanzania kwa sehemu yetu tumeamua kuweka kikubwa Serikali iendelee kuruboreshea Mazingira ya kufanya biashara pamoja na kuruhu taasisi za Fedha kutoa mikopo pasipo kuwa na riba kubwa.” Amesema Munisi.
Amefafanua kuwa watanzania wakumbuke kuwa wakipenda bidhaa za ndani kimsingi zinaleta na kuhifadhi utamaduni halisi wa mtanzania na mwaafrika kwa ujumla hivyo wananchi wajitokeze kwenye Banda hilo la Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi wa Kampuni ya wa asili asilia Dedan Munisi alifafanua jambo kwenye maonyesho ya 43 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Wilayani Temeke leo.picha na Mpiga picha wetu.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2FGopGu
via

