UPEPO mbaya
unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii
umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na
Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya
kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini
kilichozama katika kikao kilichofanyika juzikati, uongozi ambao ulibaki
madarakani kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya
memba waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye
sifa.
“Wamewaengua baadhi ya
wasanii ambao wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni
Devotha, Aunt na Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo
kujipendekeza upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya
wenye sifa za kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga
‘ubuyu’ kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama
wenye msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve
Nyerere ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.
Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel
Baada ya habari hizo kutua katika
rada ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa
waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:
Devotha: Mimi ndiyo kwanza
nakusikia wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho
na sielewi wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni
mwa waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo
sawa kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.
Odama
Odama: Hakuna kitu kama hicho,
wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa
taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka
kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.