NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WANA-Jukwaa la Chalinze
Tunayoitaka linaloundwa na wapenda maendeleo wa Chalinze Bagamoyo Pwani,wamemkabidhi mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete risiti ya sh. milioni 1.8 kwa ajili ya mifuko 120 ya saruji kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu,katika shule ya msingi Kibiki.
Akimkabidhi risiti hiyo ,mwenyekiti wa Jukwaa Alhaj Hamisi Nassoro, alisema mchango huo ni wa wana-Jukwaa hilo.
Alisema, Jukwaa linaundwa na wadau wa maendeleo, na kwamba wamedhamilia kupambana na changamoto za kielimu.
Aidha Nassoro aliomba fedha za maendeleo na wananchi zitumike kwa maslahi ya jamii.
“Hapa ni mwanzo wa shughuli zetu za kuipeleka mbele Chalinze yetu, lakini katika hili wana-Jukwaa tunaomba tupatiwe taarifa za kina, za uwepo wa tetesi za matumizi mabaya ya zaidi ya shilingi milioni miamoja, zinazotajwa kutumika pasipokufuatwa kwa utaratibu,” alisema Alhaj Nassoro.
Ridhiwani aliwashukuru wana-Jukwaa na kuwaomba wanajukwaa kulitumia kwa kuchochea maendeleo na sio kuwa sehemu ya kuleta migongano kwa wana-Chalinze.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PbGbqr
via