Meneja Uhusiano wa kamapuni hiyo ya simu, Alex Batekeye amesema hayo leo kwenye maonyesho ya 43 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema, wamekuwa wakikutana na changamoto katika zoezi hilo la usajili kwa watu kufika kujisajili wakiwa na vitambulivyo ambayo vina majina tofauti, yaani kitambulisho na jina alilojisajilia kwenye simu yanakuwa hayafanani na jin lililopo kwenye kitambulisho cha Taifa.
“Tunawaomba wananchi waje na vitambulisho stahiki yaani jina alilojisajilia kwenye simu ndio jina hilo hilo liwe kwenye usajili wa kitambulisho cha Taifa” amesema
Aidha amewataka wateja wao kuendelea kujitokeza kwa wingi katika banda lao hilo kwani mpaka sasa kuna madawati zaidi ya matano katika kufanya shughuli hiyo ya usajili kwa haraka zaidi, bila ya kuwaweka watu foleni.
Pia katika kuwaonyesha watanzania jinsi nchi yetu inavyoenda na maisha ya kidigitali na kuipeleka Tanzania kidigitali zaidi kampuni hiyo pia imeandaa dawati Unstance school yaani shule papo hapo na kuwataka wazazi wenye watoto wafike kwenye banda hilo ambapo wakifika hapo kuna sehemu dawati hilo lipo watajisajaili na kisha wataweza kutuma maswali na kupata majibu ya maswali yao hapo hapo kutokana na darasa ambalo mtoto anasoma.
Amesema, katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wengi na kuwa mkombozi wa elimu basi unaweza kujisajili hata ukiwa nyumbani kwa kutimia tovuti yao.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2L2ln3G
via


