VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE… KISA NJEGEKA

6 years ago82 Views

Na Khadija Seif,Globu ya jamii
NYOTA wa muziki kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Said Juma a.k.a Chege amewapa zawadi mashabiki wake kwa kuipua wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Njegeka ambayo amemshirikisha Vanessa Mdee.
Akipiga stori ya Michuzi Blog jijini Dar es Salaam Chege amesema kibao hicho ambacho tayari kina video yake amesema ameamu kumshirikisha Mdee ili kuleta ladha hasa kwa kuzingatia ni mwanadada mwenye kipaji cha hali ya juu katika muziki.
“Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na Vanessa Mdee zaidi ya miaka mitatu iliyopita lakini sasa nimefanikiwa kumshirikisha kwenye wimbo wangu mpya.Vanesa ni msanii wa kipekee na tofauti kutokana na kujitoa kwake kwenye ngoma pale anaposhirikishwa, kushauri ,ikiwezekana hata kuongeza baadhi ya vionjo na kuifanya kazi ikapendwa,”amesema.
Ameongeza mashabiki wataona ngoma yake Njegeka ilivyokuwa tofauti na ya kipekee na kwamba Njegeka maana yake ni mapenzi yasioeleweka yani ya kudanganyana.
Akizungumzia Meneja anayemsimamia kwenye shughuli zake za muziki, Chege amesema bado yupo kwenye mikono ya Meneja Said Fella lakini kwa sasa kutokana na majukumu ya kijamii inamlazimu asionekane nae kwenye mizunguko yake katika kazi za sanaa.
Wakati huo huo amesema kuwa mitandao ya kijamii ni sehemu kubwa ya kufahamiana na mashabiki wake kwani amekuwa akijifunza mengi na kujua mashabiki wake wanahitaji nini kutoka kwake.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2IJ82w7
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.