Mtandao
wa Instagram wiki hii umewapa majonzi baadhi ya watumiaji wake baada ya
kufanya operation ya kufuta akaunti feki (spammy accounts ) na hivyo
kuathiri namba ya followers kwa watu wengi.
“We’ve been deactivating spammy accounts from Instagram on an ongoing
basis to improve your experience. As part of this effort, we will be
deleting these accounts forever, so they will no longer be included in
follower counts. This means that some of you will see a change in your
follower count.” Wameandika Instagram.
Mastaa wa nje waliokumbwa
na fagio hilo la followers ni pamoja na Justin Bieber ambaye amepoteza
mashabiki (fake) milioni 3.5 sawa na asilimia 15 ya followers wake wote.
Mwingine ni Kim Kardashian ambaye amepoteza followers milioni 1.3 au asilimia 5.5 ya followers wake wote.
Rapper Mase ameamua kujiondoa kabisa Instagram siku ya Alhamis, muda mfupi baada ya kupoteza followers milioni 1.5