Tundu Lissu Anahitajika Polisi Tena na leo

Admin Updates1 year ago7 Views

 

Jeshi la polisi mkoani Arusha limewapa dhamana viongozi wa Chadema waliokuwa wanashikiliwa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Tundu Lissu huku wakiwahitaji kuripoti leo asubuhi Jumatatu Septemba 11, 2023.

Taarifa za kukamatwa kwa viongozi hao wa chama cha upinzani zilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Justine Masejo mchana Septemba 10, 2023 kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali na kuzuiwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kesho saa tatu wametakiwa kurudi polisi.

“Muda huu tunamsindikiza Lissu kwenda kwa kaka yake Wakili Alute Mungwai na viongozi wengine tutawapeleka hoteli na tumetakiwa kesho asubuhi saa tatu (Jumatatu) warudi,”amesema.

Amesema pia viongozi waliokuwa wanashikiliwa vituo vya polisi Karatu  akiwepo Katibu wa Baraza la Wanawake Taifa(Bawacha), Catherine Ruge pia wameachiwa.

Awali Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tangu alipokamatwa Lissu mchana walikuwa hawajuwi alipopelekwa.

“Tulikuwa tunamtafuta ili kujua alipo lakini usiku huu tulipata taarifa yupo Arusha ndipo tukaanza kushughulikia dhamana,”amesema

Amesema kukamatwa kwa Lissu na viongozi wote Karatu kulizuia kufanyika mkutano mkubwa wa hadhara mjini hapo.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.