Trump apokea barua kutoka kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Special Correspondent6 years ago7 Views

Trump apokea barua kutoka kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anatarajia kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwa mara ya pili katika hatua ya Washington kuendelea kutafuta mbinu za kuifanya Korea Kaskazini kuachana kabisa na silaha za nyuklia.

Trump amesema hivi karibuni alipokea barua “nzuri” kutoka kwa Kim Jong-un, akidai kuwa Marekani  imepiga hatua kubwa katika mazungumzo na Pyongyang bila ya kueleza maudhui ya barua hiyo.

“Tulianzisha uhusiano mzuri sana, mambo mazuri yanayotokea,” Trump aliwaambia waandishi wa habari katika White House.

“Tulifanya mkutano na Kim miezi sita iliyopita huko Singapore. Tunaweza kuwa na mkutano mwingine.Ningependa kukutana na vilevile yeye anataka kukutana.”

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya hotuba ya kitaifa ya KimJong Un siku  ya Jumanne ambapo alisema kuwa atakuwa tayari kufanya mkutano tena na Trump.

Hata hivyo Kim Jong Un ameonya kuwa Pyongyang inaweza kufuata “njia mpya” ikiwa Washington haitoondoa vikwazo vyake dhidi ya Korea Kaskazini.

Majadiliano kati ya Marekani  na Korea ya Kaskazini yamekwama kutokana na shinikizo la kiuchumi lililowekwa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini.

Nchi hiyo imeitaka Washington kuondoa vikwazo dhidi ya nchi yake lakini Marekani imesisitiza ya kuwa itafanya hivyo pale tu silaha zote za nyuklia zitakapotokomezwa.

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2Au2rDX
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.