Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) itaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Ndondo Cup 2019 kesho (Jumanne Mei 14) kwa kupambana na timu ya Rangers.
Mchezo huo umepangwan kufanyika kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Mwembe Chai kuanzia saa 10.00 jioni.
Taswa FC ambayo inafanya mazoezi mara moja kwa wiki (Jumamosi) itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza, ipo katika kundi D pamoja na timu za Ukwamani na Goba Kombaini.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamejiandaa vyema katika mchezo chini ya makocha wao, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na Saidi Seif.
Majuto alisema kuwa wanajua watapata ushindani mkali kutoka kwa timu ya Rangers, lakini hilo halitazuia kuibuka na ushindi.
Alisema kuwa kila mechi inakuwa na ushindani, lakini si kwa timu za kundi D na kuahidi kufanya vyema katika mechi zao zote.
“Tupo katika mashindano na wapinzani wetu pia wapo katika mashindano. Watashindana, lakini hawatashinda, tupo vizuri katika kila idara na malengo yetu ni kuonyesha kuwa hata waandishi wa habari nao wanaweza kucheza mbali ya kufanya kazi ya kuelimisha jamii,” alisema Majuto.
Alisema kuwa waandaaji wa mashindano ya Ndondo Cup 2019 hawakukosea kuwakubalia kushindana katika mashindano hayo ambayo mpaka sasa yamechangia kiasi kikubwa maendeleo ya soka hapa nchini.
“Nawapongeza waandaji kwa kuwa na mashindano ya soka yenye mvuto wa aina yake na kuhamasisha maendeleo ya soka,
Kuna vijana ambao wametokea katika mashindano haya na sasa wanatesa katika timu za madaraja ya juu, pia kuna wachezaji wamepata fursa ya kufanya majaribio nchi za Ulaya, hii nifaraja kubwa sana kwetu,” alisema.
Alisema kuwa wanaamini hata Taswa FC itatoa wachezaji ambao watacheza timu kubwa mbali ya kuwa ni wana- habari.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HgjKMJ
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







