Wananchi wanaoishi mikoa ya kanda ya Ziwa na mikoa ya jirani ,wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Nyakibindi, ili kujipatia elimu ya namna ambavyo teknolojia ya nyuklia inavyotumika katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo kilimo, mifugo, maji pamoja na afya.
Akizungumza katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ,Afisa mwandamizi wa Utafiti wa TAEC, Bwana Yesaya Sungita amesema kuwa wananchi watapata elimu ambayo itawawezesha kupata uelewa juu ya masuala ya matumizi salama ya teknolojia ya Nyuklia na udhibiti wake hapa nchi ili kutokuleta madhara kwa wananchi pamoja na mazingira.
Sungita amesema kuwa TAEC imekuwa ikihakikisha teknolojia ya Nyuklia inatumika ipasavyo katika sekta muhimu kama vile Maji, Mifugo na Kilimo.
Hata hivyo SUNGITA amesema mbali na wananchi kujua kuhusiana na teknolojia ya Nyuklia pia wataweza kufahamua namna TAEC inavyofanya kazi ya Kusimamia na kuthibiti matumizi ya salama ya mionzi nchini.


Timu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) katika picha ya pamoja kwnye banda lao lilipo katika uwanja wa Nyakabindi Wilayani Bariadi mkoani Simiyu ,ambapo wameanza kutoa elimu kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo namna ya teknolojia ya Nyuklia inavyotumika katika sekta ya Kilimo,Mifugo,maji na Mazingira,pia inavvyosimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Yixjpe
via
