MCHEKESHAJI maarufu nchini Masanja Mkandamizaji amesema spidi ya timu ya soka ya Simba inampa raha na kwamba mashabiki wa timu hiyo kwa sasa wanasubiri kombe lao.
Masanja ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya Simba , amesema hayo wakati anazungumzia uwezo wa timu hiyo kisoka ambapo amesema kuwa Simba inaleta raha na hasa kutokana na aina ya kandanda safi ambalo wachezaji wanalionesha wawapo uwanjani.
“Kwa kweli timu ya Simba iko vizuri sana, wanacheza kandanda la kuvutia na ukweli tumebakisha hatua moja tu kuchukua kombe,”amesema Masanja.
Mchekeshaji huyo ambaye pia ni Mchungaji , amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu uchambuzi wa soka na anavutiwa zaidi na mchambuzi Mwalim Kashasha ambaye ana aina yake ya kuchambua mpira.
“Navutia sana na Mwalimu Kashasha , anaswaga ya kuvutia sana kiasi cha kuleta hamu ya kumsikiliza,”amesema Masanja huku akisisitiza Simba iko kwenye spida ya kuchukua ubingwa tu.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Jy0wV2
via

