Soma Ratiba ya Vikao vya CCM Uteuzi wa Wagombea Wabunge

Masama BlogSIASA3 months ago179 Views

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya vikao vyake vya kitaifa ambavyo ajenda kuu itakuwa ni uteuzi wa wagombea Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge wa Viti Maalum, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Vikao hivyo vitafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 17, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Gabriel Makalla, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimepangwa kufanyika tarehe 21 Agosti 2025, kikifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kitakachofanyika tarehe 23 Agosti 2025.

Aidha, imeeleza kuwa vikao hivyo vyote vitafanyika jijini Dodoma

SOMA ZAIDI HAPA

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...