Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali yatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono jitihada za ukarabati na ujenzi kituo cha kitalii Wilayani Kongwa Jijini Dodoma ambacho kitahifadhi kumbukumbu za Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Nyerere .
Wito huo umetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipokuwa akijibu Swali la Msingi la Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde (CCM) lililokuwa likiuliza ni lini serikali itajenga maktaba yenye kumbukumbu za kazi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo kituo hicho kitakuwa sehemu ya utalii na kitajengwa Makao Makuu ya nchini ya Jijini Dodoma.
“Katika utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika,Serikali imeteua Wilaya ya Kongwa kuwa Kituo Kikuu cha Kumbukumbu za ukombozi nchini na katika kituo hicho kitakuwa na miundombinu kadhaa ya uhifadhi wa historia za viongozi ambazo zitajengwa ikiwemo kazi adhimu za Baba wa Taifa,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza wakati akijibu swali hilo la msingi Naibu Waziri huyo alisema Serikali kwa kushirikiana na UNESCO imekarabati Studio za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) zilizopo Barabara ya Nyerere na kuwa kituo adhimu cha hifadhi rejea ya kazi za Baba wa Taifa.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Shonza akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Dodoma (CCM) Felister Bura lililohoji lini ujenzi wa kituo hicho cha kumbukumbu cha Kongwa utaanza,Mheshimiwa Shonza alisema ujenzi wa kituo hicho umekwishaanza tangu mwaka 2015 ambapo ukarabati wa kituo hicho ulikwisha anza na unaendelea na pia kuna mipango mikubwa katika kituo hicho ikiwemo kujenga miundombinu ya kisasa mfano hoteli za nyota tano na kiwanja cha ndege.
Halikadhilika katika swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Tabora (CCM)Mwanne Mchemba lini serikali itaingiza katika orodha kituo cha Tabora kutambulika rasmi kama kituo cha kumbukumbu za Baba wa Taifa kutokana na historia yake na mambo aliyoyafanya Mkoani hapo,ambapo Mheshimiwa Shonza alimuhakikishia Mbunge huyo kuwa Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa Mikoa Kumi na Tano iliyoteuliwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuwa vituo vya uhifadhi wa historia hiyo.
Pamoja na hayo serikali inaunga mkono juhudi za taasisi mbalimbali zinazofanya uhifadhi wa amali za Urithi wa kumbukumbu za Baba wa Taifa na baadhi ya taasisi hizo ni Maktaba ya Taifa Dar es Salaam,Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam,Makumbusho ya Mwl.Nyerere Butiama,Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Vituo vya Televisheni vya TBC na ITV.

Naibu Waziri Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu swali la msingi bungeni la Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde (CCM) leo Mei 10,2019 Jijini Dodoma lilohoji kujegwa kwa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere katika Makao Makuu ya nchi.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vYMW4B
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






