JOSEPH MPANGALA
Serikali iko Mbioni Kujenga Kiwanda cha Mvinyo pamoja na Juise kutokana na Mabibo ya korosho ambayo yamekuwa yakitupwa mara baada ya korosho kuuzwa na hivyo Wakulima kukosa fedha za ziada kutokana na Tunda hilo.
Akiuliza swali la Nyongeza Katika Mkutano wa 15 kikao cha 29 Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe amehoji Utafiti uliokuwa ukifanywa na Chuo cha Naliendele kilichopo Mtwara kuhusu Kochoko au mabibo ya Korosho umefikia wapi Mpaka sasa kwa lengo la Kuwawezesha wakulima Kuweza kujinufaisha zaidi na zao la korosho.
“Kochoko ni zile washi zinazotokana baada ya mavuno ya korosho wakulima huwa wanazitupa na wengine huwa wanaziuza na wengine wanatengeneza Gongo na inafahamika kwamba Gongo sio pombe haramu isipokuwa namna inavyotengenezwa je Utafiti uliokuwa Ukifanywa na Chuo cha naliendele Umefikia wapi”?
Akijibu swali hilo Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kupitia Chuo cha Utafiti cha Naliendele tayari wamefanya Utafiti na kutoa maagizo ya ujengwaji wa kinu ili kuweza kuzalisha Mvinyo pamoja na juisi itakayotokana na mabibo kwa lengo la kuongeza thamani zao la Korosho.
“Ni kweli kabisa chuo chetu kupitia tawi letu la Naliendele tumefanya utafiti wa kina na tumebaini kwamba kuna mazao mengi tunaoweza kuzalisha kutokana na Korosho ikiwemo Juisi na ikiwemo mvinyo maalum unaotokana na mabibo ya Korosho na tumetoa maagizo kwenye tawi letu sasa hivi kujenga kinu cha kuweza kuchakata ili tuweze kuzalisha mvinyo pamoja na juisi ambayo tutaiuza hapa Nchini na hivyo itaongeza thamani na mapato yatakayotokana na zao la Korosho” amesema Hasunga Waziri wa Kilimo.
Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Vt5NyM
via

