Mkurugenzi wa Sharif Condition Sheikh Chief Msopa amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweza kufanya mambo ikiwemo kujenga msikiti mkubwa katika Ofisi za Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata).
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Msopa amesema kuwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli hana upendeleo wowote alichofanya ni kuweka usawa wa Dini.Amesema kuwa watu wanataka kuharibu utaratibu kwa kuanza kufikiria uchaguzi sasa wakati bado kuna maendeleo yanafanyika na Rais aliyopo madarakani.
Aidha amesema kuwa hakuna serikali inayoweza kuingiza fedha kwa kila mwananchi kinachotakiwa ni kufanya kazi tu.
Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuangalia katika kipindi kifupi maendeleo yamefanyika kwa kasi kubwa ikiwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Msopa amesema kuwa katika kipindi cha Utawala wa serikali ya awamu ya tano fursa nyingi zimejitokeza kwa ajira kwa vijana yote ni kutokana na ubunifu wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.Aidha ameunngana na Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Uhamasishaji wa usafi katika jiji la Dar es Salaam.Amesema mkutano wa SADC ni mkubwa hivyo usafi ufanyike na kuwa endelevu.
Mkurugenzi wa Sharif Condition Chief Msopa akizungumza na waandishi habari kuhusiana maendeleo yanayofanyika katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ylHaLt
via

